Tragedy

George Tyson atimiza siku 40 toka afariki dunia,Monalisa amtumian ujumbe ‘Ur angel is smiling now’

Muongozaji mkongwe wa filamu nchini, George Tyson leo ametimia 40 toka afariki dunia May 31 kutokana na ajali ya gari maeneo ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma, ambapo aliyekuwa mke wake Monalisa amemtumia ujumbe.

monalatyson
Monalisa akiwa na marehemu Goerge Tyson enzi za uhai wake pamoja na mtoto wao

Kupitia Instagram Monalisa ameandika: George,40 days toka ulipoondoka..mengi yametokea mmh! I wish ungefumbua macho dakika tu uone, unakumbuka ile story ulinihadithia ulitaka kuiandika tuifanye movie ukaipa jina la ‘When I come back ‘ yaani kama ulijitabiria, mwanzoni nilikuwa nadhani ni sinema unatuchezea lakini nimeamini You are no longer with us, But ur Angel is smiling now,wala usiwe na hofu we know upo kwenye mikono salama, tunakuombea na maisha yetu yanaendelea najua hicho ndicho kitu ungependa kukiona kwetu ingawaje juzi tuliitwa na @tv1tanzania nilipofika pale nikashindwa kujizuia, tutakukumbuka daima @jojityson”

Baada ya kifo chake mwili wake ulisafirishwa hadi Dar es salaam kwaajili ya kumuaga na baada ya hapo mwili ulisafirishwa kwenda kwao Kenya kwa mazishi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents