Habari

Gereza la Keko latozwa faini kwa uchafuzi wa mazingira

Gereza la Keko la jijini Dar es Salaam limetozwa faini ya shilingi milioni 30 kwa kutiririsha maji taka yenye athari kwa afya za wananchi.

Pia naibu waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, ameziagiza taasisi za serikali zikiwemo gereza hilo na kiwanda cha kutengeneza madawa cha Keko na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kutupa taka ovyo na kutiririsha maji taka sehemu zisizo rasmi.
luhagampina

Naibu waziri huyo ametoa agizo hilo akiwa ziarani katika manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

“Lakini utiririshaji huu kama mnavyouona wameulalamikia wananchi lakini hata kungekuwa hakuna wananchi hapa wanaoishi hii sheria ya mazingira hairuhusu namna yoyote ya utililishaji wa maji taka kama unavyofanya na gerza hili,”alisema Mpina.

Aidha Mpina ameiagiza mamlaka ya usimamizi wa mazingira (NEMC) kwa mkuu wa gerza hilo kujenga miundo mbinu ya maji taka ambayo ni rafiki kwa mazingira sambamba na kulipa faini hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents