Burudani

Guchi afanya kweli, aachia ngoma mbili kwa mpigo

Staa wa muziki kutoka Nigeria anayesumbua vichwa vya wasanii wengi kwa kizazi kipya kwenye Afrobeat, Guchi ameachia vyuma vizito viwili ambavyo ni ALL OVER YOU na MON BEBE, ambapo ALL OVER YOU  imetengenezwa na Shugavybz huku MON BEBE ikiwa imetengenezwa na Kaelbeatz.

Ngoma hizi ambazo zinazungumzia mapenzi zimejawa na story tofauti ambapo kwenye  ngoma ya ALL OVER YOU anazungumzia mahusiano yalivyo mlewesha na yupo tayari kupambana na kushikamana hadi kufa kwenye mahusniano hayo,

Kwa upande wa ngoma ya MON BEBE ambayo imetayarishwa na Kaelbeatz, Guchi ama unaweza muita Purple girl… anaelezea utamu anaoupata kwa mpenzi wake ikiwemo kupata vipele vidogo vya mapenzi kila anapomuona. Kwenye ngoma zote mbili mrembo huyo ni kama anatoa story ya mfululizo ya mapenzi iliyopo juu yake.

Kitendo hiki cha Guchi kuachia kazi zote mbili kumetajwa kuwa ni cha upendo kwani anaweza kufanya kama alivyofanya  2022 kwenye EP yake ya PURPLE DIARY? Au la amewatunuku tu mashabiki zake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents