Michezo

Hasheem Thabit aikacha NBA atimkia Japan

Mtanzania, Hasheem Thabit amepata nafasi ya kujiunga na klabu ya Yokohama B inayoshiriki Ligi Kuu ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini Japani.

Thabiti ambaye ni mchezaji wazamani wa klabu ya Oklahoma City Thunder inayoshiriki ligi ya Marekani ‘NBA’ ataanza kuwatumikia waajiri wake hao wapya huku akiwa na uzoefu mkubwa na mchezo huo.

Wakati ligi ya mpira wa kikapu nchini Japan ikitarajiwa kuanza hapo kesho siku ya Ijumaa mtanzania huyo ameamishia maisha yake huko kwa sasa.

Wakati akipata chakula cha usiku mchezaji huyo amesema kuwa “ Nimejifunza mambo mengi kuhusiana na ushindi na hakika tutashinda natutakuwa juu ya wote,” amesema Thabit.

Jumbe mbalimbali katika mitandao ya kijamii ya nchini Japan ikimkaribisha mtanzania, Hasheem Thabit katika ligi ya mpira wa kikapu ambapo atakuwa anavalia jezi nambari 34.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents