Burudani

Reality Tv show ya Idris Sultan kuanza kuoneshwa December BET, aeleza sababu za kuchagua kituo hicho cha Marekani

Kama mipango ya mshindi wa Big brother Africa 2014, Idris Sultan ikienda vizuri basi dunia itashuhudia show mbili mpya za Tv za star huyo wa Tanzania kupitia channel ya Marekani- BET

Idris mkasi

Idris amesema moja ya show hizo ni reality show kama ilivyo ya kina Kim Kardahsian, KUWTK na Husbands Of Hollywood, na nyingine ni ya comedy.

Show hizo zitakua zikioneshwa kupitia BET na kituo cha runinga cha Vuzu.

Idris amesema sababu kubwa za kuamua kuichagua BET, ni kwasababu anataka kuingia kwenye soko la Hollywood kwa haraka.

“Zimeshakuwa recorded na kila kitu, tulivipeleka mara ya kwanza wakatupa marekebisho ya kufanya…Kuna kama channel kadhaa ambazo zinaweza zikachukua.” alisema Idris kupitia 255 ya Clouds Fm.

Ameongeza kuwa mpaka kufika mwezi December show hizo zitakuwa zimeanza kuoneshwa na vituo hivyo.

“Mpaka kwenye mwisho wa mwaka huu ndio zinaweza kuanza kuwa aired”.

Lugha itakayotumika kwenye show hizo ni Kiswahili na Kiingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents