Burudani

Imeniuma: Alikiba aeleza kusikitishwa baada ya vyombo vya habari kupuuzia kushiriki kwake kwenye ‘Peace One Day’

Alikiba ameeleza kusikitishwa kwake kwa kile alichosemwa kupuuzwa kwa ushiriki wake kwenye kampeni ya Peace One Day iliyofanyika jana kwenye uwanja wa Amohoro jijini Kigali, Rwanda.

11850301_174173629585951_1534969192_n

Alikiba aliungana na wasanii wengine wa Afrika wakiwemo Mafikizolo, Ice Prince na wengine kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani kwa kutumbuiza wimbo wao maalum.

11939356_1042179599149845_1814231293_n
Picha aliyoweka Alikiba kwenye ujumbe wake

“Hii ni kwa vyombo vya habari ambavyo havijatoa ushirikiano katika kampani ya peace one day,” ameandika kwenye Instagram.

“Next time fanya kwaajili ya Tanzania sio kwasababu ya Alikiba au mtu yoyote atakayewakilisha Tanzania kwasababu mimi ni binaadam sijakamilika naweza kuwa nimekukosea bila kujua au kwa kujua pia.”

“Haijalishi kwasababu nchi yetu ina amani ndio muache kutoa ushirikiano kumbukeni tupo kwenye kipindi kigumu cha uchaguzi naomba Mungu atunusuru kwa hilo lakini pia inaleta picha mbaya kwa nchi za jirani zenye machafuko kuona hatutoi ushirikiano,” ameeleza.

“Kwahiyo haipendezi kwa kweli. Kuna wapenzi wa kazi yangu wamelalamika sana kila kona ya dunia kuhusu kampani ya peace one day kwanini hamkuona hilo !! imeniuma.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents