Habari

iPhone 5 yamdhuru mwanamke mwingine China, baada ya kumlipukia wakati anaongea na simu aliyokuwa anai ‘charge’

Mwanamke mmoja nchini China anadaiwa kulipukiwa na simu yake aina ya iPhone 5 na kumuumiza machoni baada ya kuongea na simu kwa muda mrefu huku ikiwa kwenye charge.

iPhone5

Mwanamke huyo Li, kutoka kaskazini mashariki mwa China, alisema alihisi simu yake imechemka sana baada ya kuzungumza na simu hiyo kwa dakika 40 na baada ya kujaribu kukata simu ilikataa kukatika na ghafla ikalipuka na kupata mpasuko kwenye kioo upande wa kulia juu.

Li alisema vipande vidogo vya kioo cha simu hiyo iliyolipuka vilimrukia machoni na kumdhuru, iliripoti Want China Times.

iphone5_unboxing2

Hili ni tukio la pili kuripotiwa ndani ya miezi miwili kutoka China likihusisha matukio ya kufanana baada ya lile la msichana Ma Ailun, (23) aliyeripotiwa kufariki mwezi mmoja uliopita baada ya simu yake ya iPhone 5 aliyokuwa anaongelea huku ikiwa kwenye chaji kumpiga shoti.

Wiki iliyopita kampuni ya Apple ilitangaza tahadhari juu ya kuwepo kwa bidhaa nyingi bandia sokoni na kutoa ofa ya charger original kwaajili ya bidhaa zake kama iPhone, iPad,iPod kwa punguzo la nusu bei ili kukabiliana na bidhaa hizo bandia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents