Burudani

Janet Jackson akatisha maandalizi ya ‘The Unbreakable World Tour’ ili kumuuguza baba yake aliyepatwa na kiharusi

Muimbaji wa R&B Janet Jackson amelazimika kukatisha maandalizi ya ziara yake ya dunia iliyopewa jina la ‘The Unbreakable World Tour’ kufuatia baba yake Joe Jackson kupatwa na kiharusi.

JJ and father

Janet ambaye ni mke wa bilionea wa Qatar, Jumanne wiki hii alisafiri kwenda Sao Paulo, Brazil alikolazwa baba yake.

Mzee Jackson alilazwa baada ya kupata kiharusi (stroke) Jumamosi iliyopita ambayo alikua akisheherekea birthday ya kufikisha miaka 87.

Inadaiwa kuwa Janet atakuwa na baba yake mpaka hali yake itakapokua nzuri ndio atarejea katika shughuli zake za kimuziki.

JJ anatarajia kufanya show 36 katika ziara hiyo Iliyopangwa kuanza August 31.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents