Burudani
Jay Z, Beyonce, Nicki Minaj, Usher na mastaa wengine kutumbuiza kwenye show ya charity ya Tidal
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2015/10/tidal.jpg)
Baada ya mtandao wa Tidal kufikisha zaidi ya watumiaji milioni moja, Jay Z aliahidi kusheherekea na sasa ametangaza shangwe hizo zitakuwa lini na wapi.
Jay ametangaza show za charity za TIDAL X: 1020 ambapo kwa mara ya kwanza itafanyika Oct. 20 kwenye uwanja/ukumbi wa Barclays Center, Brooklyn.
Pamoja na Jay Z mwenyewe, mastaa wengine watakaotumbuiza ni pamoja na Beyoncé, Prince, Nicki Minaj, Usher, Lil Wayne, na T.I. Wengine ni Nick Jonas, Damian Marley, Fabolous, Alessia Cara, Bas na Justine Skye.
Tiketi za show hiyo zitauzwa kuanzia $74 na $244. Show hiyo itaonekana live kupitia TIDAL.com na HTC.com.