Habari

Jeshi la Polisi nchini Uganda lawaomba radhi wananchi kwa kumpiga Mwandishi wa Habari

Baada ya video ikiwaonesha Askari Polisi nchini Uganda wakimshushia kichapo Mwandishi wa Habari wa shirika la utangazaji la Reuters nchini humo, James Akena kusambaa mitandaoni. Hatimaye Jeshi hilo limeomba radhi kwa kitendo hicho.

IGP Martin Okoth Ochola

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo IGP Martin Okoth Ochola amesema kuwa Jeshi la polisi kazi yake ni kuhakikisha raia wake wanakuwa salama kwa kuwalinda na sio kuwanyanyasa kama video hiyo mtandaoni inavyoonesha.

Nimepata mafunzo ya Uchunguzi na Upelelezi (CIP) kwa zaidi ya miaka 10, nimelitumikia pia jeshi la polisi kwa miaka 3o lakini sijawahi kumnyanyasa wala kumpiga raia. Nashangaa kwanini polisi wanamtesa raia? jukumu lao ni kumkamata tena bila hata ya kumpiga kwani hata wao wanajua kitendo hicho ni kosa kisheria na kinyume na maadili ya Upolisi,“amesema IGP Ochola.

IGP Ochola amesema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho na amewaomba radhi wananchi kwa niaba ya jeshi la polisi na tayari ameeleza kuwa Polisi wawili wanashikiliwa tayari kwa kupelekwa mahakamani.

Akena alipigwa na kujeruhiwa vibaya na polisi wakati wa maandamano ya wananchi mjini Kampala wakipinga kitendo cha kukamatwa  Mbunge wa jimbo la Kyadondo, Bobi Wine ambaye pia ni mwanamuziki mkubwa nchini humo.

Related Articles

25 Comments

  1. Ila yule wa kwetu Tz hapa hakuombwa radhi na jeshi la polis kwa kipgo kile eti wanasema yy ndio alkosea asehh Tz shikamoo, najua hampnd onekana mmekosea ila Mungu anawaona hzo gwanda hamtoingia nazo mbinguni na mkizikwa nazo zitaoza tu chini kwa chini

  2. KWAKWELI INATIA HURUMA SANA KWA SERIKALI ZETU ZA AFRIKA ,SIJUI UNAKUA NI UCHOCHEZI WA MARAISI WETU ,NA NILAZMA IWE IVO ,JESHI ANATUMIA ORDER TU ,KUWENI NA URUMA NA NDUGU ZENU ,ICHO KITI KINA MWANZO NA MWISHO WAKE ,,,SHIDA SANA NA UZUNI KWA SISI RAIA WA KI AFRIKA TUNAO ISHI AFRIKA

  3. Kwani wao walivyo anzakumpiga hawakufikiria kama kumpigamtu kunamazarayake kisha eti wanaombamsama sasa msayakazigani upumbavu mtupu kwamaana hata uyo raisi waomwenyewe mjingatu. Anafikiria huo u president ataishinaomilele. Awaulize Nyerere waukowapi Mandela. Mobutu nawengine waache raiya watetee hakizao siowanafanya ujinga

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents