MichezoUncategorized

Mfahamu mwanamichezo wakike mwenye mkwanja mrefu zaidi duniani 

Bingwa mara 23 wa Grand Slam, Serena Williams ametajwa na Forbes kuwa ndiye mwanamichezo wa kike anaye miliki mkwanja mrefu zaidi duniani.

Williams alilipwa dola 62,000 mwaka uliopita baada ya kuwa nje kwa miezi 14 kujifungua lakini alijizolea dola milioni 18 kutoka kwa matangazo ya biashara.

Moja kati ya nyumba za Serena Williams

Katika horodha ya wachezaji 10 wa kike wenye mkwanja mrefu zaidi wawili pekee ndiyo hawatoki katika mchezo wa tennis

Mchezaji wa Badminton PV Sindhu na mwendesha magari Danica Patrick ndio wanaspoti wasio wachezaji tenisi walio katika orodha ya kumi bora.

Mwezi Juni Forbes iliwaorodhesha wanaspoti 100 wenye kipato cha juu zaidi lakini hakukuwa na mwanamke kwenye orodha hiyo baada ya Williama kukosa kuorodheshwa.

Mwanamasumbwi Mmarekani Floyd Mayweather alichukua nambari moja akifuatwana mchezaji soka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo

Mwanaspoti wa kike ambaye alipata kipato cha juu zaidi alipokea dola milioni 105 kwa jumla kutoka Juni 2017 hadi Juni 2018.

Mapato ya Williams yanamweka nafasi ya kwanza kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Caroline Wozniacki yuko nafasi ya pili baada ya kushinda ubingwa wa Grand Slam kwenye mashindano wa Australia Open, ushindi uliompa dola milioni 3.1 na kuongeza kipato chake hadi pauni milioni 13.

Rais wa Urusi Sharapova alikuwa mwanaspoti wa kike aliyekuwa na kipato cha juu zaidi kwa miaka 11 mfululizo lakini kipato chake kimeshuka kufuatia marufuku ya miezi 15.

Wanaspoti 10 wenye kipato cha juu zaidi

  1. Serena Williams (tennis) – $18.1m (£14m)
  2. Caroline Wozniacki (tennis) – $13m (£10.1m)
  3. Sloane Stephens (tennis) – $11.2m (£8.7m)
  4. Garbine Muguruza (tennis) – $11m (£8.5m)
  5. Maria Sharapova (tennis) – $10.5m (£8.1m)
  6. Venus Williams (tennis) – $10.2m (£7.9m)
  7. PV Sindhu (badminton) – $8.5m (£6.6m)
  8. Simona Halep (tennis) – $7.7m (£6m)
  9. Danica Patrick (mbio za magari) – $7.5m (£5.8m)
  10. Angelique Kerber (tennis) – $7m (£5.4m)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents