Burudani

Akaunti ‘fake’ ya Instagram inayotumia jina la Jokate yamtoa povu Irene Uwoya!

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na akanti nyingi ‘fake’ za Instagram ambazo zinatumia majina ya mastaa na viongozi wa serikali na usipokuwa makini unaweza kugombana na kila mtu mtandaoni. Kwani akaunti hizo zimekuwa zikitumiwa na watu hao kwaajili ya kuwachonganisha mastaa kwa mastaa ili wapate followers.

Hayo yamemkuta malkia wa filamu, Irene Uwoya baada ya kuingia kwenye majibizano na akaunti ‘fake’ ambayo inatumia jina la Jokatemwegeelo akidhani anabishana na Mhe DC Jokate, ambae kupitia mtandao huo anatumia jana Jokate Mwegelo.

Kaunti hiyo ‘fake’ ilionekana ikidai muigizaji huyo wa filamu amekuwa akitumia muda mwingi kwenye kujiremba na sio kufanya kazi.

Akaunti orijino ya DC Jokate

Baada ya kauli hiyo, Irene Uwoya aliamua kumjibu mtu huyo akidhani anajibizana na Jokate na kama unavyoona kwenye screenshot hapo juu.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents