Habari

Sakata la wanawake waliotelekezwa Dar, Joyce Kiria atinga kwa RC Makonda (+Video)

Mwanaharakati wa masuala ya usawa wa kijinsia na Mtangazaji wa kipindi cha ‘Wanawake Live’, Joyce Kiria ni moja ya mamia ya wanawake waliojitokeza leo Jumatatu Aprili 09, 2018 kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kupatiwa msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa na waume zao.

Akiongea nje ya Ofisi hizo, Joyce Kiria amesema kuwa mwaka huu heshima kati ya wanawake na wanaume lazima iimarike kwani wanaume wengi wamekuwa wakiwatelekeza wanawake baada ya kuwazalisha.

Mwezi Januari mwaka huu, Joyce Kiria aliutangazia umma kuwa yeye na mumewe Henry Kilewo hawapo kwenye maelewewano kwani amekuwa akiitunza familia peke yake.

Soma zaidi – Mjasiriamali Joyce Kiria amwaga siri za mumewe hadharani ‘nimebeba mzigo’

Mwezi Machi 22, 2018. Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda alitangaza kuwa wawanake wote waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto kufika ofisini kwake leo Jumatatu ya April 09, 2018 kwaajili ya kupatiwa msaada wa kisheria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents