Burudani

Mjasiriamali Joyce Kiria amwaga siri za mumewe hadharani ‘nimebeba mzigo’

Mwanaharakati na mwanamke shujaa nchini Tanzania, Joyce Kiria ameweka hadharani kuwa mahusiano yake kwa sasa na mumewe Henry Kileo ambaye alishawahi kushika nyazifa mbalimbali CHADEMA kuwa hayapo sawa.

Joyce Kiria na mumewe Henry Kileo siku yao ya harusi.

Joyce Kiria amesema kuwa kwasasa mahusiano yake hayapo sawa kwani yeye amekuwa ndiye baba na mama wa familia kwa kila kitu yaani kuhudumia familia nzima pamoja na mumewe.

Akitoa taarifa hiyo kwa umma kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akibubujikwa na majozi, Kiria amesema huwa anamshauri mumewe atafute japo kazi itakayowaingizia kipato ili kusaidiana kutunza familia lakini mumewe anakuwa mkali na kumpiga.

Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanyua kunipiga (@kilewo2020mwanga) ukasahau kabisa! ukasahau yooote. Nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote, Malipo yako ni kunipiga/ kunidhalilisha na kunitoa machozi, umenipiga kwa sababu Mimi ni mnyonge siyo! sina nguvu, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME. Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali, ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ni nini? kuniua??,“ameandika Kiria huku akielezea jinsi alivyompigania mumewe hadi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 hadi akaingiza deni kubwa na kufungiwa kipindi chake cha Wanawake Live kilichokuwa kinaruka EATV.

Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua, kama ni mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote Mungu yupo. Leo umenipiga (@kilewo2020mwanga)?? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni mwanaume kwa kunipiga.“amemaliza Kiria.

Mumewe na Joyce Kiria ni moja ya vigogo wa CHADEMA na kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Mwanga, Kilimanjaro lakini kwa bahati mbaya alishindwa kupata nafasi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents