Michezo

Jurgen Klopp asikitishwa na mashabiki Liverpool kuondoka uwanjani kabla ya mechi kumalizika

Kocha Jurgen Klopp baada ya kopoteza mechi yake ya kwanza baada ya kuchukua mikoba ya Brendan Rogders baada kufungwa na timu ya Crystal Palace mashabiki wa Liverpool waliamua kuondoka uwanjani na walimuacha peke yake kocha Jurgen Klopp mara baada ya mlinzi wa Crystal Palace, Scot Danny kufunga goli la ushindi katika dakika ya 82 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 2-1.

article-3309492-2E42F33300000578-88_964x406

Akiongelea tukio hilo baada ya mchezo huo kumalizika, kocha huyo raia wa Ujerumani alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha mashabiki kumkimbia na kumuacha peke yake wakati timu ikihangaika kurudisha bao, hali anayoisema kuwa alijihisi mpweke zaidi na kusikitishwa sana na tukio hilo.

Klopp-2

Klopp amewataka mashabiki kuwa wavumilivu na kwamba haipendezi kutoka uwanjani kabla ya dakika ya mwisho kwani kwenye mpira lolote linaweza kutokea na kwamba ni vizuri kuisapoti timu hadi mwisho.

Klopp alishuhudia kuumia vibaya kwa mlinzi wake wa kati Mamadou Sakho ambaye atafanyiwa scan kuona ni muda gani atakua nje ya uwanja.

Klopp amesema ni heri apoteze mechi hata kwa bao 3-1 kuliko kumpoteza mchezaji kwa majeruhi, kwani kwake mchezaji ndiye muhimu zaidi kuliko matokeo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents