Burudani

Kala Jeremiah asema ‘Nchi ya Ahadi’ ni wimbo unaotakiwa kusikilizwa na kila Mtanzania

Rapper Kala Jeremiah anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Nchi ya Ahadi’ unaopeleka ujumbe kwa Rais, Mawaziri, Wabunge na kwa wananchi wote wa Tanzania.

20150310042505

Kala ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo aliomshirikisha Roma Mkatoliki ni wimbo ambao kila mtanzania anahitaji kuusikiliza ili kujua hatma yake.

“Idea ilikuja kwa kuona mambo mbalimbali na kuangalia hali ya maisha ya watanzania. Kwahiyo nchi ya ahadi mimi nadhani niwaombe kuanzia mheshimiwa rais, mawaziri, wabunge, wafanyakazi wote, wananchi wa kawaida walio na ajira na wasio na ajira, wakulima, wachoma mkaa yaani watu wote kwa ujumla, wasikilize wana kitu chao wanakihitaji kipo kwenye wimbo,” amesema.

“Kwahiyo niwaambie watanzania wote kwa ujumla huu ni wimbo wao wanatakiwa wausubirie na utakuwa unapatikana bure kwenye mitandao na watausikia kwenye radio. Kila mtanzania anatakiwa kuusikiliza ili kujihakikishia yeye ni mtanzania na anahitaji mambo mbalimbali pamoja na hatma yake. Sitaki kuzungumzia ndani zaidi lakini ni wimbo mzuri. Roma amepita sehemu yake na mimi pia, kwahiyo mashabiki wasubirie wiki ijayo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents