Burudani

Katika marapa wa kike Tanzania, Tiffah Flow namba moja – One The Incredible

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, One The Incredible amefunguka na kueleza kuwa kwa mtanzamo wake Tiffa Flow ndiye msanii namba moja kwa rap Bongo kwa upande wa wasanii wa kike.

One ambaye anatamba na ngoma ‘Put It On Me’ ameiambia The Playlist ya Times FM licha ya kuwa msanii yeye ni shabiki wa hip hop hivyo anajua vingi katika muziki huo.

“Kwanini naamini Tiffah Flow ni rapper bora kabisa, kwa sababu ndiye MC pekee wa kike Tanzania hii, yeye na Stosh, unaweza ukafanya naye ngoma na usitegemee ataandika kitu gani,” amesema.

“Ninachukulia nipofanya ngoma na mtu kama Tiffah au Stosh ni sawa sawa ninapofanya ngoma na mtu kama Young Killer, nategemea kutakuwa na utunzi fulani wa ziada,” amesisitiza.

Soma Pia: Mjue Real Mama Tiffah

Katika hatua nyingine One amesema ‘mvutano’ wa maneno ulikuwa kati yake na rapa Chemical anahisi ni baada ya kutompatia nafasi kwa biti ambazo alikuwa amezitengeneza Mpo Africa Studio lakini kwake anaona kilikuwa kitu cha kawaida hasa kwa upande wa biashara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents