Michezo

Kazuyoshi Miura aweka rekodi mpya Japan

Kazuyoshi Miura ambaye ni raia wa Japani kwasasa ana umri wa miaka 50, ameweka rekodi mpya kuwa mtu wa umri mkubwa zaidi kufunga bao katika mechi ya soka ya ushindani. aliweka rekodi hiyo kwa kufunga bao la pekee wakati wa ushindi wa 1-0 wa Yokohama FC dhidi ya Thespa Kusatsu katika ligi ya daraja la pili nchini Japan.


Kazuyoshi Miura alifunga mabao mawili mechi 20 alizocheza msimu uliopita, nyingi akiingia kama nguvu mpya kipindi cha pili

Rekodi ya awali iliwekwa mwaka 1965 na Mwingereza Stanley Matthews, aliyefunga bao lake la mwisho mechi ya ushindani akiwa na umri wa miaka 50 na siku tano.

Miura anamzidi umri kwa siku tisa.

Miura, ambaye aliwahi kuchezea timu ya taifa ya Japan na kuwafungia mabao 55 katika mechi 89, kwa sasa anacheza soka msimu wake wa 32.

Alistaafu soka ya kimataifa miaka 17 iliyopita.

Miura wakati mmoja alicheza soka ya kulipwa Ulaya.

Alianza uchezaji wake akichezea Santos ya Brazil na akacheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa mwaka 1986.

Alichezea Genoa na Dinamo Zagreb miaka ya 1990.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents