Habari

Kenya yaitaka Uingereza iwachukulie hatua polisi wake waliomtesa Mkenya (+Video)

Kenya imeiandikia Uingereza ikidai haki juu ya ukatili dhidi ya raia wa Kenya unayodaiwa kufanywa na maafisa wa polisi katika eneo la Colchester, Essex nchini humo.

Tukio la ukatili huo lilichukuliwa kwenye picha ya video ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuibua hasira na vilevile kuchochea vugu vugu la ‘Black Lives Matter’ dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Katika video hiyo, polisi takriban sita wa Uingereza wanaonekana wakimtesa Mkenya aliyetambuliwa kama Wycliff Cox walipokuwa wakitaka kumkamata kwa madai ya kukiuka sheria za dhamana.

Maafisa hao wanaonekana wakikandamiza kichwa cha Wycliff ardhini huku wakishikia shingo yake, huku watu wa familia yake ikitazama na mama yake akisikika akiomba : “Usimuue kijana wangu.”

Huku uso wake ukionekana kutoka damu, mikono na miguu ikiwa imefungwa, Wycliff, ambaye ameripotiwa kuwana ugonjwa wa akili, anaonekana akichukuliwa na polisi na kuingizwa ndani ya gari la polisi lililokuwa linasubiri.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu , Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza ulitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya mafisa hao kwa ‘’matumizi ya nguvu zisizo za lazima kwa mtu ambaye hakuwa na silaha.

“Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza umepokea video ya kusikitisha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo polisi katika Colchester, Essex wanaonekana wakimtesa Mkenya , Bw. Wycliff Cox,” alieleza taarifa ya ubalozi wa Kenya nchini Uingereza:

https://www.instagram.com/tv/CGR-apyBo4K/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents