Bongo Movie

Kesi ya Wema Sepetu yapigwa kalenda hadi Julai 10

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeharisha kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Bangi inayomkabili Msanii wa filamu, Wema Sepetu na wenzake hadi Julai 10, mwaka huu.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde Jumatano hii alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa shauri hilo lilipaswa kuanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Thomas Simba lakini hayupo.

Mkunde alidai kuwa Hakimu Simba ameanza likizo, hivyo anaomba shauri hilo liahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa alisema kuwa shauri hilo limeahirishwa hadi Julai 10, mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusilizwa.

Mbali ya Wema, katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida ambapo wanakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa hizo.

Awali wakiwasomea maelezo ya makosa yao, Wakili wa Serikali, Constatine Kakula alidai Wema alikuwa ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Alidai Februari 3, mwaka huu, alijipeleka kituo cha polisi cha kati ambako alikamatwa na Februari 4, mwaka huu, ukaguzi ulifanyika nyumbani kwake ambapo kulipatikana vitu vinavyodhaniwa dawa za kulevya.

Kakula alidai ukaguzi huo ulifanyika mbele ya msanii mwenyewe, polisi na shahidi huru na Februari 6, mwaka huu, vitu hivyo vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na Februari 8 mkemia alitoa taarifa ya uthibitisho juu ya vielelezo hivyo kuwa ni bangi yenye uzito wa gramu 1.08.

Alidai Februari 8, mwaka huu, Wema alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa mkojo, ambapo uchunguzi ulieleza mkojo wa msanii huyo ulikuwa na bangi.

Katika maelezo hayo ya awali, Wema alikubali majina yake, mahali anapoishi na kwamba alikuwa miongoni mwa waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kujihusisha na dawa za kulevya.

Pia alikibali kujipeleka polisi huku akikana maelezo mengine. Washitakiwa wengine walikubali majina yao na kuwa wafanyakazi wa Wema.Kesi imeahirisha hadi Juni 14, mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents