Habari

Kifaa kinachodhaniwa kuwa kinalipuka chabainika nyumbani kwa Barack Obama na Hillary Clinton

Kifaa kinachosadikiwa kuwa ni mlipuko kimebainika katika nyumba kwa Hillary Clinton na  Barack Obama hii leo, maafisa wa sheria wameiviambia vyombo vya habari nchini Marekani.

Aina kama hiyo ya kifurushi kinachoshukiwa kimetaarifiwa kutumwa pia katika jengo la Time Warner jijini New York.

Ni siku mbili baada ya bomu kurushwa katika nyumba ya mfadhili na mshauri wa mambo ya fedha George Soros huko mjini New York.

The Time Warner building in New York City was evacuated on Wednesday morning

Clinton ambaye ni rais wa zamani wa Marekani na mke wake Bi.Clinton ambaye aliwania urais mwaka 2016. Taarifa zilizoripotiwa na New York Times zimesema kwamba kituo hicho kilibainika kuwa kinalipuka baada ya fundi kukifanyia uchunguzi.

Kifaa hicho kiliachwa kilomita 65 kaskazini mwa mji wa New York.

Obama

Haijawekwa wazi kuwa kifaa hicho kinachotiliwa shaka kilionekana wapi.

Kwa mujibu wa shirikisho la habari la BBC, msemaji wa Obama amekana kuwepo kwa tukio hilo na kuwataka waandishi kushirikiana na idara ya huduma ya maelezo ya siri.

Maafisa wakuu wa White House wameiambia NBC kwamba rais Donald Trump tayari ameshapata taarifa kuhusu jambo hilo.

Msemaji wa Ikulu Sarah Sanders amelaani jaribio hilo la mashambulio ya vurugu dhidi ya watu mashuhuri.

“Matukio ya kigaidi hayakubaliki popote na mtu yeyote ambaye atakamatwa kuhusika atachukuliwa sheria

Uchunguzi bado unaendelea ili hatua sahihi ziweze kuchukuliwa” Msemaji wa Whitehouse Sarah Sanders .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents