Burudani

Kifo cha Mzee wa Mjegeje chazua gumzo

Mchekeshaji maarufu aliyejipatiia umaarufu kupitia mitandao ya kijamii Umar Lahbedi Issa maarufu Mzee wa Mjegeje amefariki dunia jana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam. Akiongea na waandishi wa habari.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja wa Mzee wa Mjegeje, Clement Charles amesema “Mimi Mzee wa Mjegeje nilisimama kama Meneja wake nilikuwa namuomgoza kwenye kazi zake za sanaa na hata mara ya kwanza kufanya kipindi na Millard ilikuwa ni Mimi namsimamia, msiba umetokea jana saa 7 alikuwa anasumbuliwa na ini lilifeli na figo, maziko yanafanyika leo saa 10 Keko Madukani” “Mzee wa Mjegeje ameacha Mtoto wa Kike mmoja ila Mwanamke aliachana nae”.

Itakumbukwa Mzee wa Mjegeje aliwahi kufanya kazi na Wasanii mbalimbali ikiwemo kushiriki kwenye video ya wimbo wa Msanii Harmonize.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents