Habari

Kijana alipa mahari baada ya mkewe kufariki

Kijana mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane alilazimika kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikiendi iliyopita. Kulingana na chombo cha habari cha taifa, mkewe alifariki kutokana na tatizo ya kujifungua.

Ndugu wa marehemu walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuafikia majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya kufariki.

Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yaliyozuiliwa yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefariki, kukubali kulipa zaidi ya dola 800 na kufanya harusi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.

Ndugu wa kijana huyo Irmao do Jovem alielezea kuwa walijaribu kuchangisha fedha zilizokuwa zinahitaji na waliweza kupata dola 178 pekee, na fedha zilizobakia walihaidi kulipa siku ya harusi.

By PeterAkaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents