Michezo

Kijana aliyeshinda dola milioni 2.2 kwa bahati nasibu Kenya

Kijana wa miaka 28 ambaye ni mzaliwa wa Kakamega, magharibi mwa Kenya ndiye wa kwanza kujishindia kiasi kikubwa cha pesa kwa kubeti barani Afrika

Kijana huyo ambaye alibashiri kwa ufasaha matokeo ya mechi 17 mwishoni mwa wiki, amejishindia jumla ya Sh.221m za Kenya, ambazo ni sawa na dola 2.2m za Marekani.

Mshindi huyo wa Mega Jackpot ya kampuni ya Sportpesa alianza kushiriki mashindano ya bahati nasibu ya kubashiri matokeo mwaka jana, baada ya kutambulishwa kwa mchezo huo na nduguye.

Baada ya kuibuka mshindi wa pesa hizo kijana huyo kwa sasa amepelekwa eneo salama kutokana na wasiwasi kwamba huenda watu wakafika kwa wingi kumpongeza au pengine kutaka kufahamu siri yake.

Kijana huyo alikuwa tayari ameanza kusherehekea alipogundua kwamba alikuwa amebashiri vilivyo matokeo ya mechi 14 kati ya 17 zilizokuwa kwenye Mega Jackpot pale alipopigiwa simu na afisa mkuu mtendaji wa Sportpesa Ronald Karauri muda mfupi baada ya saa sita usiku.

Mechi ambazo mshindi alibashiri kwa ufasaha matokeo yake:

Sunderland v Bournemouth
Stoke City v West Ham
West Bromwich v Leicester
Barnsley v Burton
Bastia v Rennes
Guingamp v St Etienne
Metz v Nancy
Montpellier v Lille
Caen v Marseille
Bologna v Udinese
Empoli v Sassuolo
Everton v Chelsea
Augsburg v Hamburger SV
Dijon v Bordeaux
Tottenham Hotspur v Arsenal
Inter Milan v Napoli

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents