Habari

Kikosi cha usalama barabarani chakusanya mamilioni ndani ya siku 3(+Video)

Kikosi cha Usalama barabarani, Kanda Maalum ya Dar es salaam cha ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kimekusanya takribani jumla ya milioni 304,590,00 kwa siku 3.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro, amebainisha hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo alisema wanaendelea vizuri.

“Suala la usalama barabarani tangu tarehe 22.5.2017 hadi tarehe 25.5.2017 kwa siku takribani 3 tumeweza kukusanya takribani jumla ya milioni 304,590,00/= kwahiyo tunaendelea vizuri,” alisema Kamanda Sirro.

Tazama video:

Hata hivyo kwa siku hizo tatu idadi ya makosa ilikuwa hivi : Magari yaliyokamatwa 9,127, Pikipiki zilizokamatwa 498, daladala zilizokamatwa 3,839,Magari mengine(binafsi na Malori) 5,288, bodaboda waliofikishwa Mahakamani kwa makosa ya kutovaa helment(kofia nguvu) na kupakia mishkaki 30, jumla ya makosa yaliyokamatwa 10,153.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents