Habari

Kimbunga ‘JOBO’ chaimarika, TMA yatoa ushauri kwa Wananchi

Mamlaka ya Hali ya Hwe Tanzania (TMA) imetoa taarifa juu ya mwenendo wa kimbunga ‘Jobo’ ambacho kwa sasa kinadaiwa kuwa umbali wa kilomita 410 kutoka pwani ya Mkoa wa Lindi.

”Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “Jobo” kilichopo bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.
Kimbunga Jobo kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya nchi yetu kimbunga hiki kinatarajiwa kuwa
umbali wa takriban kilomita 410 kutoka pwani ya mkoa wa Lindi. Hata hivyo, kimbunga Jobo kinatarajiwa kupungua nguvu yake kadri kinavyosogea katika pwani ya Tanzania.”- Taarifa kutoka TMA.

TMA imesema kuwa uwepo wa kimbunga Jobo utaathiri mifumo ya hali ya hewa ”Aidha, izingatiwe kuwa uwepo wa kimbunga Jobo unatarajiwa kutawala na kuathiri mifumo ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kusababisha vipindi vya ongezeko la mvua na upepo mkali katika maeneo ya ukanda wa Pwani.”

Hata hivyo Mamla hiyo imetoa ushauri kwa Wananchi  ”Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hiki na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa zake mara kwa mara kila inapobidi.”

Kwa mujibu wa mashirika ya Kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952. Ripoti zilziotolewa hapo jana zilisema kimbunga hicho kilionekana kaskazini mwa Madagascar kikiwa na kasi ya kilomita 83 kwa saa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents