Michezo

Kinda wa Arsenal Alex Iwobi agombewa na England na Nigeria zamng’ang’ania

Mchezaji wa klabu ya Arsenal Alex Iwobi ambaye pia timu ya taifa ya England iko mbioni kumzuia nyota huyo asijiunge na timu ya Super Eagles ya Nigeria.

325D0DF800000578-3504017-Iwobi_celebrates_having_scored_his_first_goal_for_the_Gunners_du-a-1_1458639403472

Hii inafwatia kauli ya chipukizi huyo ya kuasi timu ya taifa ya Uingereza na badala yake kujiunga na vigogo wa soka ya Afrika Super Eagles ya Nigeria.

Iwobi ameshajumuishwa katika kikosi cha Nigeria kinachoratibiwa kuchuana dhidi ya Misri siku ya Ijumaa 26 -29 Machi katika mechi ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika.

England imeanza harakati za kumshawishi asijiunge na Nigeria kwani hilo litawanyima fursa ya kumshirikisha katika timu ya taifa ya England.

Iwobi mwenye umri wa miaka 19 aliichezea England katika mashindano ya dunia ya vijana wasiozidi umri wa miaka 16,17 na hata 18 kabla ya kuamua kuwa angependa kuiwakilisha taifa alikozaliwa yaani Nigeria kuambatana na kanuni za FIFA.

Jarida la Daily Mirror linaripoti kuwa harakati za kimya kimya zinafanywa ilikumshawishi Iwobi abadilishe kauli yake kabla ya Ijumaa, kwani akishaichezea Super Eagles itakuwa vigumu mno kuichezea England katika mechi za kimataifa.

Iwobi amejumuishwa katika timu ya kwanza ya klabu yake ya Arsenal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents