Michezo

Klabu ya Simba SC yatupwa nnje kombe la Shirikisho na Coastal Union

Robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania (Federation Cup) imepigwa kati ya Coastal Union dhidi ya Simba katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na huku coastal Union ikifanikiwa kuitoa Simba katika michuano hiyo kwa ushindi wa Bao 2-1.

IMG_5917

Magoli ya coastal yamefungwa na Mchezaji wa Cameroon Youssouf Sabo,huku goli la Simba likifungwa na Mganda Hamisi Kiiza.

Coastal sasa inajumuika na Yanga, Azam FC na Mwadui kwenye Droo ya kupanga Mechi za hatua ya Nusu Fainali itakayofanyika Jumanne .

Mshindi wa Michuano hili ataiwakilisha Tanzania mwaka 2017 katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents