Habari

Kleyah: Muimbaji aliyetosa kazi nzuri ya UNDP kwa mapenzi ya muziki

Kleyah ni msanii anayefanya vizuri na wimbo wake ‘African Drum’ huku video yake iliyoongozwa na Justin Campos ikichezwa kwa wingi kwenye kituo cha MTV Base. Nilizungumza naye kwenye Chill na Sky kutaka kumfahamu zaidi.

10311196_229349697413071_320289790_n

Alizaliwa na mama Mtanzania na baba mwenye asili ya Rwanda na Uganda na kusoma katika shule mbalimbali ikiwemo kumaliza shahada ya Mawasiliano kwenye chuo kikuu cha Phoenix, Arizona nchi Marekani. Kabla ya kwenda huko alikuwa akisoma kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.

Ameishi pia nchini Namibia.

Baada ya kumaliza masomo yake alikuja nchini Tanzania ambapo alipata kazi nzuri kwenye shirika la maendelea la umoja wa mataifa, UNDP ambako alifanya kazi kwa miaka mitatu kabla ya kuamua kuacha ili kuendelea career yake ya muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=-VlBY73LBMk&app=desktop

Anatarajia kuachia album yake mwaka huu. Msikilize zaidi hapo chini kwenye Chill na Sky.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents