Burudani

Kolabo na Alikiba ilivyompatia Nuh Mziwanda Mjengo

Msanii wa muziki Bongo, Nuh Mziwanda amesema kolabo yake na Alikiba ‘Jike Shupa’ ilimuwezesha kufanya tour Tanzania nzima.

Nuh Mziwanda amelazika kueleza hilo ikiwa ni jibu kwa wale waliokuwa wakisema nyumba aliyonesha kuwa ni yake haikuwa kweli. Muimbaji huyo amesema fedha za ujenzi wa nyumba hiyo zilitoka kwenye tour alizokuwa akizifanya.

“Nyumba ni yangu na katika ujenzi nilikuwa namshirikisha sana mama yangu, yeye ndio aliyekuwa anashughulika na mafundi. Mimi sikuwa nafuatilia, kipindi kile ndio nilikuwa nimeachia Jike Shupa, nilifanya tour Tanzania nzima, chaka to chaka wilaya kwa wilaya,” amesema.

“Nilikuwa nikipata pesa yangu kidogo kidogo namtumia mama anajenga, kwa hiyo mimi narudi huku nakuta nyumba imefika sehemu nzuri kwa sababu nakumbuka nilikaa miezi mitatu,” Nuh ameiambia Wasafi TV.

Ngoma ya Jike Shupa ambayo ilitoka June 2016 ndio ngoma pekee kutoka kwa Nuh Mziwanda kufikisha views zaidi ya Milioni 2 katika mtandao wa YouTube. Pia Jike Shupa ndio wimbo wa mwisho kwa Nuh kumshirikisha msanii mwingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents