Habari

Kuhifadhi Maiti Morogoro hadi Moro Mjini – Babu Tale

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale @BabuTale

Ameipongeza Serikali kwa kazi nzuri ya kuboresha Sekta ya Afya Jimboni kwake ikiwemo kupeleka Ambulance Kituo cha Afya Mkuyuni lakini hata hivyo amesema Jimbo hilo halina chumba cha kuhifadhia maiti hivyo kupelekea Mtu anapofariki maiti kwenda kuhifadhiwa Morogoro Mjini. Akiongea Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tale amesema “Tunamshukuru Mh. Rais kwa kutuletea Vituo vya Afya lakini hatuna sehemu ya kuhifadhia maiti leo hii tukipata maiti Morogoro Kusini Mashariki lazima tukahifadhi Morogoro Mjini sasa samahani kwa kusema hivi Mtu anaona Mtu ana rest in peace lakini hapa ana-rest na stress, Mtu umefiwa halafu bado utafute gari ya kwenda kuhifadhi maiti Mjini” “Mh. Mchengerwa tunakuomba ufike Morogoro Kusini uone changamoto zetu”.

 

 

 

 

 

CC: Millard ayo.

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents