BurudaniHabari

Wadudu sio Wahalifu – RPC Masejo

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linalo wajibu wakisheria wa kuwalinda raia na mali zao huku likibainisha kuwa limepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa Ulinzi wa Mkoa wa Arusha Mh. Paul Makonda aliyoyatfoa hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo kufuatia maagizo ya Mkuu wa Mkoa ambapo alilitaka Jeshi la Polisi Mkoani humo kuimarisha Ulinzi na Usalama ili kuwezesha Biashara na shughuli nyingine za Utalii kufanyika kwa ndani ya saa 24.

Akizungumzia Vijana maarufu Jijini Arusha, Wadudu OG, Kamanda Masejo amesema kuwa Vijana hao siyo wahalifu bali ni kionjo cha jiji la Arusha.

“Hawa wanaojiita Wadudu ni vijana ambao ukiwatazama ni kama wasanii kwa maana wanafanya sanaa, wanapeleka Ujumbe kwa hiyo ukiwatazama kwa jicho tofauti unaweza kuwaelewa tofauti lakini siyo hivyo.

“Kama mkuu wetu wa Mkoa alivyozungumza (Makonda) alisema kuwa ni wewe tu unavyoweza kuwatumia. wale Vijana kimsingi ni Wasanii mimi nawachukulia kama moja ya vionjo cya Arusha na silo Wahalifu.

“Kuna kundi ambalo wao wanajiita Wadudu Orijino uhalisia wao utakuta wanavaa viatu vikubwa, suruali kubwa, wanapeleka ujumbe wao sio Kundi la Uhalifu.

“Lakini wengine wanapenda kuendesha Pikipiki kwa kiasi na madoido, ambayo RC amesema hii ni sanaa pia kwa hiyo si kama watu wanavyotafsiri” amesema Kamanda Masejo.

 

 

 

 

 

CC:Tanzaniaweb.Live

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents