Burudani

Kuna vitu vingi ambavyo nimefanya kama wa kwanza lakini huwa sipendi kuji-proud – Wakazi

Wakazi ni rapper ambaye ameshafanya vitu vingi vya kuweka rekodi kama msanii wa kwanza Tanzania kufanya lakini hapendi sana kujitangaza, kitu kinachofanya watu wasijue na wakati mwingine kumkosesha kupata pongezi anazostahili.

wakazi

“Kusema kweli sipendagi kujiproud, kuna vitu vingi ambavyo nimefanya kama wa kwanza,” alisema Wakazi kupitia kipindi cha Full Charge cha Pride Radio Mtwara.

“Mbona mimi ni msanii wa kwanza ambaye alikuwa hajulikani nika perform Big Brother, msanii wa kwanza ku perform Nigeria. Mwaka 2014 February nimefanya show tatu nimefanya show na kina Davido kule.” alisema Wakazi.

Aliendelea;

“So kuwa wa kwanza kufanya kitu fulani ni nzuri na unawafungulia watu lakini sio lazima muda wote ujikweze, ofcourse hili swala la Tidal limesababisha watu wengine wameniuliza umefanyaje then unamwelezea msanii mwenzako anafanikiwa kuweka hivyo wote Watanzania tunakuwa tuko wengi tunautangaza muziki wetu.”

Wakazi ni miongoni mwa wasanii wa mwanzo wa Tanzania kufanikiwa kuweka muziki wake kwenye mtadao wa Tidal unaomilikiwa na Jay Z.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents