Burudani

Kwa Dogo Janja nimekipata nilichokuwa nakitaka – Irene Uwoya

Muigizaji Irene Uwoya amesema tangu ameolewa na Dogo Janja amekuwa akisumbuliwa na baadhi ya watu kwa kufikiri wanaweza kupata hiyo nafasi kama msanii huyo lakini yeye hapo ndio amefika.

Irene Uwoya ameiambia Leo Tena ya Clouds Fm kuwa watu hao ingawa hapo awali walikuwepo lakini baada ya kuolewa ndipo usumbufu umezidi kisa umri wa Dogo Janja.

“Toka nimeolewa watu wengi wamekuwa wakisumbua japo hapo mwanzoni walikuwepo lakini kwasasa kuna aina ya watu ndiyo wamekuwa wakisumbua kwa kuhisi sababu Abdul kanioa basi hata wao wanaweza kupata nafasi hiyo” amesema.

Kuhusu tofauti ya umri kati yao, Irene Uwoya amesema, “Ni kweli nimemzidi Dogo Janjatz umri ila kwangu umri ni namba maana nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na watu ambao wamenizidi umri au tupo sawa lakini sikupata nilichokuwa nakitaka lakini kwa mume wangu nimekipata,”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents