BurudaniLady Jay Dee
Lady Jaydee kuzindua ‘M.O.G Bar & Restaurant’ October 31, iliyokuwa ‘Nyumbani Lounge’
Lady Jaydee ametangaza jina jipya la sehemu ambayo Machozi Band ilikuwa ikitumbuiza na kufahamika kama Nyumbani Lounge.
Kupitia Instagram Jide ameshare poster ya uzinduzi wa ‘M.O.G Bar & Restaurant’ ambayo zamani ilikuwa ikifahamika kama ‘Nyumbani Lounge’.
“Narudi kazini rasmi Baada ya miezi 4 ya uvivu. Karibuni tar 31 October M.O.G 82 Ada Estate, Tranic Plaza Pale pale” ameandika Jide.