Burudani

Lady Jaydee: Naamini nitakuja kupenda tena (video)

Lady Jaydee yuko nchini Kenya, na miongoni mwa vitu vilivyompeleka ni pamoja na kufanya media tour kwenye vyombo mbalimbali vya habari kupromote kazi yake mpya ‘Give Me Love’.

Jide na Tuva
Willy Tuva na Lady Jaydee

Akiwa katika mahojiano na Willy M. Tuva wa Radio Citizen kupitia kipindi maarufu cha Mseto Mseto, Jide aliulizwa kuhusiana na sababu za kuvunjika kwa ndoa yake, ambazo aliwahi kuzieleza katika mitandao ya kijamii. Alipoulizwa kama bado anaamini katika mapenzi na kama ana mpango wa kuolewa tena, hili lilikuwa jibu lake:

“Aaaah sina ukakika […] mapenzi hua yapo, lakini unapokuwa umetoka kwenye mahusiano kidogo roho inarudi nyuma, lakini sisemi kwamba hakuna mapenzi, mapenzi yapo ndio maana ukapenda, ukakaa halafu tena labda yakashindikana ukapenda tena, kwasababu sio kwamba hiyo (na Gadner) ni relationship yangu ya kwanza […] niliwahi kuwa tena na boyfriend nyuma nikapenda nikavunjwa moyo yakaisha, nikapenda tena, kwahiyo naamini nitakuja nipende tena.”

Tazama mahojiano hayo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents