Habari

Lowassa aeleza alichozungumza na Rais Magufuli baada ya kukutana naye

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amefunguka na kueleza kitu alichozungumza na Rais Dk John Pombe Magufuli baada ya kukutana naye hivi karibuni kwenye hafla ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
LM
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa wakati wa hafla ya maadhimisho ya Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa .

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Lowassa amesema hakuwa na nguvu ya kukataa mkono wa mkuu huyo wa nchi licha ya chama chake kuwa kwenye mgogoro mzito wa maneno ya serikali.

“Jibu ni rahisi sana, hatukuongea lolote la msingi zaidi ya kusalimiana na kutakiana heri,” alisema Lowassa. “Nani miongoni mwenu mkristu ambaye atatoka rais wa nchi kwenye kiti chake aje aseme tutakiane amani alafu ukatae mkono. Tena mbele ya macho ya Kadinali, maaskofu na wakristu wengi wengine, nani niongoni mwenu atakataa mkono,”

Aliongeza, “Sikuwa na nguvu ya kukataa mkono huo, niliupokea , tulikaa pamoja tukasalimiana, tulihaidiana kuwasiliana, nangojea mawasiliano. Kwa hiyo kwa kifupi yalikuwa ni hayo,”

Wiki chache zilizopita katika mazishi ya Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif alikataa mkono wa salamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dr.Ali Mohamed Shein.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents