Burudani

Lupita Nyong’o aanza misele na mpenzi wake mpya raia wa Nigeria

Lupita Nyong’o ameonekana kwa mara ya kwanza akiwa na mpenzi wake mpya mwanamitindo mwenye asili ya Nigeria, Mobolaji Dawodu.

Lupita
Lupita akiwa na mpenzi wake Mobolaji Dawodu

Wawili hao wameonekna Jumanne hii kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja kwenye mchezo wa tennis kwenye mashindano ya US Open huko jijini New York wakati Serena Williams alipokuwa akicheza na Ekaterina Kakarova.

Siku chache zilizopita Lupita alithibitisha kuwa na mahusiano na mwanamitindo huyo huku akidai kuwa amemua kumweka mahusiano yake mitandaoni baada ya kumchunguza kwa muda wa miezi sita.

Dawodu ni mwanamitindo lakini pia ni muhariri wa jarida la mitindo GQ la nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents