Habari

Madereva walioendesha wakiwa mtungi siku ya mwaka mpya wajikuta mbaroni

Madereva kibao wamekamatwa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuendesha magari huku wakiwa wamelewa katika sikukuu ya mwaka mpya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema walifanya operesheni dhidi ya madereva na kuwabaini madereva hao wamekuwa wanakunywa huku wakiendesha ambapo ni kinyume na sheria.

“Sasa hivi tukimkamata dereva akiwa amelewa hatumuandikii faini ya kulipa tumeona wengi tumeona wengi wao wameona rahisi kuendelea kurudia makosa,hivyo tunawapeleka mahakamani sheria ichukue mkondo wake,” alisema Kamanda Sirro.

Aidha Kamanda Sirro alisema katika operesheni hiyo waliwakamata madereva 10 Temeke,15 Kinondoni na Ilala 4 .

BY:EMMY MWAIPOPO

CHANZO: MWANANCHI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents