HabariSiasa

Mahakama yaamuru Zuma arejeshwe jela

Mahakama ya rufaa nchini Afrika Kusini imesema leo kuwa kutolewa gerezani kwa rais wa zamani Jacob Zuma kwa msamaha wa kimatibabu kulikuwa kinyume cha sheria, na kwamba anatakiwa kurudishwa jela kukamilisha kifungo chake.

Zuma mwenye umri wa miaka 80, alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela mwezi Juni mwaka jana kwa kosa la kuidharau mahakama, hatua iliyozua machafuko nchini humo. Hata hivyo, alitumikia kifungo cha miezi miwili pekee kabla ya kupewa msamaha kutokana na sababu za kiafya.

Msamaha ulitolewa na mkuu wa huduma ya magereza nchini humo, licha ya kamati ya matibabu kusema Zuma hakukidhi masharti ya kupewa msamaha huo.

Kulingana na ripoti za kimatibabu zilizotajwa katika uamuzi wa mahakama ya rufaa, Zuma ana matatizo ya shinikizo la damu, viwango vya juu vya sukari na vidonda vya utumbo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents