Bongo5 Makala

Makala: Sura tatu za Harmonize ndani ya WCB (+Audio)

Ni miaka minne sasa tangu msanii Harmonize awe chini ya label ya WCB, kwa kipindi chote hicho ameweza kuonesha ufundi wa aina yake katika utunzi, kuimba na kutumbuiza.

Ndiye msanii wa kwanza kusaini katika record label hiyo na wimbo wake wa kwanza kutoa ni Iyola. Kadiri siku zinavyozidi kwenda amezidi kukua katika kiwango chake.

Harmonize wa mwaka huu ni tofauti na yule wa mwaka uliyopita na miaka mingine. Kutokana na ukuaji wake ambao umechangiwa na jitihada zake ameweza kuonesha sura tatu ndani ya label hiyo. Karibu kumsoma.

1. Kolabo Nyingi Afrika

Ukimtoa Diamond Platnumz ni wazi Harmonize ndiye msanii anayeongoza kufanya kolabo na wasanii wengi wa nje (wa kimataifa) ndani ya WCB.

Ameweza kuwashirikisha na yeye kushirikishwa pia, hivi ndivyo msanii anakua na kipimo cha kukubalika na wenzie na si yeye kuwatumia kama njia ya kufikisha muziki wake mbali zaidi pasipo kuwasaidia na wengine.

Kwa mwaka 2017/18 ameweza kufanya kolabo na wasanii kutoka nchi mbali mbali, ameweza kufanya na Marina kutoka Rwanda, Yemi Alade kutoka Nigeria, Eddy Kenzo kutoka Uganda, Emma Nyra kutoka Nigeria, Willy Paul kutoka Kenya, IYO kutoka Nigeria na OmoAkin kutoka Nigeria

Kolabo yake na rapper kutoka Ghana, Sarkodie ‘DM Chick’ inaonesha ni kwa kiasi gani anahitaji kukua na kutangaza muziki Afrika nchini.

Hivi karibuni alipokuwa katika media tour nchini Kenya, Harmonize alisema imefika kipindi wasanii kufanya muziki kwa ajili ya bara zima la Afrika.

Utakumbuka kabla ya kutoa ngoma na Sarkodie mwaka jana alitoa ngoma na Korede Bello kutoka nchini Nigeria, hivyo mwaka huu amepiga hatua moja zaidi ukiangalia uzito wa jina la Sarkodie na Korede Bello katika muziki wa Afrika.

2. Fedha

Diamond Platnumz anamtaja Harmonize kama msanii wenye fedha nyingi zaidi ndani ya WCB kwa sasa.

Katika kipindi ch The Playlist kinachoruka Times FM, Diamond alisema kuwa Harmonize ni miongoni mwa wasanii ambao anajua wana fedha katika label yake, hivyo akawa amethibitisha hilo ambalo lilikuwa likizungumzwa kwa muda mrefu.

“Naweza kusema kama wasanii wangu waliokuwepo WCB, msanii mwenye hela ni Harmonize, muziki wake una riziki kubwa,” alisema Diamond.

Hata hivyo Harmonize anaeleza kuwa ni kitu kizuri ila sio vizuri kukaa kwenye media na kusema kuwa una fedha kwani anaimbia watu ambao wapo mtaani na wengine hata kula yao ni shida, hivyo kwa namna moja au nyingine inapunguza mashabiki.

“Mimi sina pesa hizo ila kidogo ninachopata Mwenyenzi Mungu ninashukuru, na lakini mimi pia ni msanii nafanya show hivyo kwa namna moja napata riziki,” alisema Harmonize pia katika pindi hicho.

Harmonize anataja show zake kama sehemu ambayo inamuingiza fedha zaidi, mfano ni show aliyofanya Kenya hivi karibuni ambayo anaeleza kulipwa zaidi ya Tsh. Milioni 20. Pia anatarajia kuanza tour nchini humo hivi karibuni na mwezi wa nane ana tour nchini Marekani.

Pia anaweka wazi kuwa YouTube ni sehemu ambayo inamuingiza fedha zaidi, kwa kipindi cha miaka miwili (2016-2018) ameingiza zaidi ya Tsh. Milioni 270. Kutokana na hayo yote kulipelekea kuibuka stori huenda na yeye amewekeza ndani ya Wasafi TV.

Hata hivyo alipoulizwa iwapo na yeye ni miongoni mwa wamiliki wa Wasafi TV alisema si kweli ila kila mmoja anayetazama ni mmiliki wa chombo hicho.

3. Kolabo na Diamond

Utakumbuka August 26, 2018 wasanii wote wa kutokea WCB walikutana katika ngoma moja inayokwenda kwa jina la Zilipendwa.

Licha ya kolabo hiyo kuna wasanii kama Harmonize na Rich Mavoko walikuwa wameshamshirikisha Diamond katika nyimbo zao, huku ukimjumlisha Rayvanny katika orodha hiyo ila yeye alishirishwa na Diamond katika wimbo ‘Salome’.

Hata hivyo Harmonize amekuwa na bahati ya kipekee kwani ameweza kumshirikisha Diamond katika ngoma zake mbili kitu ambacho hamna msanii wa WCB aliyefanya hivyo.

Wimbo wa kwanza walitoka mwaka 2016 ambao ulikwenda kwa jina la Bado na wimbo wa pili ‘Kwa Ngwaru’ umetoka mwaka huu. Hizi ni nyimbo zenye mafanikio makubwa zaidi kwa upande wa Harmonize.

Kwa mfano wimbo wa Bado ndio wimbo wa Harmonize wenye views wengi zaidi katika mtandao wa YouTube, hadi sasa una viwes zaidi ya milioni 18.3. Wakati Kwa Ngwaru ikiweza kufikisha viewes milioni 10 ndani ya mwezi mmoja na kumfanya Harmonize kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya hivyo.

Kwa hayo machache ndivyo unaweza kumtazama Harmonize kwa sasa ndani ya WCB, vitu hivyo vinamfanya kutazamwa kwa jicho la tofauti na wale mashabiki zake katika maana nzuri yenye kujenga katika muziki na maisha ya kawaida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents