Bongo Movie

Malick kufunga ndoa na Rose Ndauka hivi karibuni

Msanii wa filamu nchini Rose Ndauka na mpenzi wake Malick Bandawe aka Chiwaman wamesema kuwa maandalizi ya ndoa yao yamekamilika na kinachosubiriwa kwa sasa ni siku ya kufunga ndoa.
Chawaman akiwa na Rose Ndauka

Akizungumza na bongo5 leo, mpenzi wa Rose, Chiwaman ambae ni baba wa mtoto mmoja na Rose, amesema ndoa yao ipo siku za usoni baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.

“Familia inaendelea vizuri tu, dogo ameshakuwa vizuri sasa hivi, anaweza fanya fujo mbili tatu, siyo kama imeishiwa wapi ,kitu ambacho kilichokuwepo mbele yetu ni ndoa, ni kujitayarisha tu kwa wale watakao pata kadi , watu wengi tu watapata kadi tutakaa tuka,enjoy , ndo yetu kila kitu kimeshapangika , tukianza kusambaza kadi kila mmoja atajua ni tarehe ngapi ,mimi naomba nisiliongee, ni hivi karibuni, kama kila kitu kimepangwa basi ujie ni soon” Alisema Chiwaman

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents