Promotion

Mama Lishe, Tandi Boi wageuka wamiliki magari ya Airtel Yatosha Zaidi

SIKU ya wapendao kwa kwa mwaka huu wa 2015 huenda ikawa ni siku ya kukumbukwa zaidi katika maisha ya wateja saba wa huduma zinazotolewa na kampuni ya simu za mkononi nchini ya Airtel Tanzania, kwani siku ilikuwa ni ya kwanza kwa wateja hao kuwa wamiliki wa magari mapya ya kifahari.

10985257_916523968379362_5249233109813721898_n

Airtel, kupitia promosheni yake iliyojipatia umaarufu mkubwa kwa sasa, saa chache kabla ya mkesha wa Siku ya Wapendao, Ijumaa iliyopita, ilifanya droo kutafuta washindi wa wiki wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi, na ndipo, miongoni mwa washindi hao saba, Mtanzania mjasiriamali ambaye ni mamalishe, Sakina Mshamu Libwana mkazi wa Kiwalani, Dar es Salaam na tandiboi/kondakta, Justin William wa Tabata hapa hapa jijini, walipojinyakulia Toyota IST mpya kutoka Airtel.

Balozi wa Airtel Yatosha, msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu, ndiye aliyekuwa na jukumu la kuwafahamisha na kuwapa taarifa za ushindi huo wateja hao wa Airtel wakati wa droo hiyo iliyofanyika makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa mwakilishi wa Bodi ya Michezo Kubahatisha Tanzania, Hemed Abdallah.

Ilikuwa ni furaha kwa Lulu na wageni wengine waalikwa wakati mmoja wa washindi hao, Sakina, ambaye ni mamalishe, aliposhindwa kuendelea na mazungumza kwa njia ya simu baada ya kutaarifiwa kwamba yeye sasa ni mmiliki wa Toyota IST mpya kwa sababu tu ya kuingia katika huduma ya Airtel Yatosha.

“Kweli? Unasema kweli dada? Asante sana na wala siamini Mungu wangu…,” alisema Sakina na kukata simu kwa furaha huku akimwacha Lulu akiendelea kumpa maelekezo na kujikuta akiongea peke yake kwenye simu hiyo.

Mbali na hao wawili, wateja wengine watano walioshinda magari hayo na kutaarifiwa na Lulu ni pamoja na mganga wa tiba asilia, Said Mashiko kutoka Katavi, Edson Mwamsasu (mkulima, Kyela), Hamim Yoyo (msusi, Korogwe, Tanga) na Ester Mashauri, muuguzi wa Hospitali ya Bugando, Mwanza na Ibrahim Sasya Kimolo wa Arusha

Akizungumza wakati wa kuchezeshwa kwa droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema: “Hadi sasa ni magari 10 tu kati ya 60 yaliyotengwa kwa ajili yako wewe mteja wa Airtel ambayo yamepata wamiliki.

“Bado kuna magari 50, unajuaje kama wewe hautakuwa mmoja wa wamiliki wa magari haya 2015? Endelea kujiunga na Airtel yatosha zaidi kwa kupiga namba *149*99# na kuchagua kifurushi unachokitaka.

“Lakini, jambo muhimu zaidi kwa wateja wa Airtel leo niawapa msisitizo kila ijumaa droo inachezwa jioni hivyo wateja msizime simu zenu ili msipoteze Bahati zenu za kumililiki magari” alisisitiza Mmbando.

Promosheni hii ya kuvutia ilizinduliwa takriban wiki moja tu iliyopita na tayari wateja 10 wa Airtel wameshinda magari hayo mapya.
“Cha ajabu zaidi ni kwamba, kumbe hata watu wa chini kama sisi tunaweza kushinda promosheni. Mimi nilidhani hizi huwa ni dili za wajanja Fulani wenye nafasi zao manake nchi hii tunaijua,” alisema Mashiko kutoka Katavi.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents