Habari

Mamilioni ya wahindu leo waondoa nuksi kwa kujitosa ndani ya mto Ganges

Mamilioni ya waumini wa madhehebu ya Hindu nchini India wamejitosa katika mto wao mtakatifu wa Ganges, kitendo ambacho wanaamini kinawaosha dhambi zote.

Siku ya leo inachukuliwa kama siku yenye heri kubwa zaidi katika maadhimisho ya siku 55 yajulikanayo kama Kumbh Mela, ambayo umuhimu wake unatokana na masuala ya kinajimu.

Afisa Mkuu wa maadhimisho hayo Mani Prasad Mishra amesema tayari watu milioni tatu wamekwishaingia ndani ya mto Ganges kuanzia asubuhi na kwamba wanategemea kuwa ifikapo jioni watu milioni kumi na moja watakuwa wamejiosha na maji ya mto huo yenye baridi kali.

Wakereketwa wa dini ya Hindu wanaamini kwamba kuoga ndani ya mto Ganges kunaondoa dhambi zao, na kuwaepusha na mzunguko wa kifo na kuzaliwa kwa mara ya pili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents