Michezo

Manula,Bocco na Said Ndemla wala tuzo mbele ya Ubalozi wa Uturuki

Klabu ya soka ya Simba hapo jana imewapatia tuzo wachezaji wake ambao wamefanya vizuri kufuatia michezo mbali mbali waliyo cheza.

Katika ghafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovutoglu pamoja na Mkewe Bi. Yeşim Meço Davutoglu walimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mlinda lango namba moja ndani klabu ya Simba, Aishi Manula.

Lakini pia balozi, Ali Dovutoglu aliwakabidhi medali wachezaji bora wa mechi nne zilizopita nahodha John Bocco na Kiungo Said Ndemla ambao walishinda kufuatia kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Singida United, Kagera Sugar, Ndanda FC na Majimaji FC.


Tuzo hizi zimetolewa katika hafla maalumu iliyoandaliwa na Ubalozi wa Uturuki kwa ajili ya kujenga na kuimarisha ushirikiano mzuri kati ya klabu ya Simba na nchi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents