Burudani

Mapacha (Rappers) wadai wana amani moyoni kumaliza mgogoro na Clouds FM, ‘beef imeturudisha nyuma’

Rappers wa kundi la Mapacha, wamesema kwa sasa wana amani moyoni baada ya kumaliza tofauti yao na uongozi wa Clouds Media Group.

993803_619942598053027_1180125411_n

Mapacha wamesema waliamua kwenda kwa Mkurugenzi wa Vipindi na Utayarishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kuomba kumaliza tofauti zao za miaka mingi zilizoanzishwa na movement ya Vinega na Anti Virus kwakuwa waligundua ugomvi haukuwa na faida yoyote kwao.

Akiongea na kipindi cha Showtime Next Chapter cha RFA, jana, member wa kundi hilo, Dotto aka D wa Maunjanja Saplayaz, alisema ni wao wenyewe ndio walioamua kufanya hivyo kwa manufaa ya maisha yao.

“Kuna vitu vingine vya msingi vya kuvifanya na sio hii tu. Idea ilikuwa ni sisi wenyewe twende tukaongee nao kwamba ‘bwana hii beef ni tunaimaliza, tunaweka mambo yote clear kwamba sisi tuko poa na hatuna nanihii yoyote tuendelee na mambo mengine’,” alisema.

D alikiri kuwa ugomvi wao na Clouds FM uliwaharibia mambo mengi katika maisha na mipango yao na ndio sababu kubwa ya wao kuona si muhimu kuundeleza.

“Kwa upande wetu sisi, imetuharibia vitu vingi kwasababu vitu vingi tulikuwa tunafuatiliana zile. Kwasababu unaweza ukapata show sehemu fulani, unashangaa ile show mara wanaingiza siasa mnakuwa mnashindwa kwenda kufanya show. Au mnaenda kuomba sehemu fulani mfanye show watu wanawaogopa ‘hawa jamaa nini na nini, si unajua zile? Ni vitu vingi tu inatuharibia. Halafu kuna wasanii wengi hawataki kufanya kazi na sisi, kwahiyo tunakuwa tunashindwa kuendelea.”

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents