Habari

Martha Mwasu Waziri awa Mama Shujaa wa Chakula 2012

Bi. Martha Mwasu Waziri akisherehekea ushindi wake

Martha Mwasu Waziri jana usiku alishinda shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012.

Bi. Waziri amejishindia zawadi ya shilingi milioni 10 za kitanzania ambazo atazitumia kununua vifaa vya kilimo atakavyotaka mwenyewe.

Martha anatokea mkoani Dodoma ambako kwa kutumia njia za utunzaji wa mazingira alizojifunza kutoka kwa Inades Formation, aliweza kuikoa ardhi yenye ukubwa heka 18 iliyokuwa imeharibika kwa mmomonyoko wa udongo na kugeuza kuwa shamba lenye ardhi yenye rutuba.

Martha anasema angependa kuifundisha elimu aliyoipata alipokuwa kwenye kijiji cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula na ana ndoto za kuligeuza shamba lake kama la mfano kuwaonesha wengine kile kinachotakiwa kufanywa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents