Mitindo

Marufuku kuvaa miniskirts Uganda, wabunge wapitisha muswada wa ‘anti-pornography’

Wabunge wa nchini Uganda leo wameupitisha muswada wa ‘anti-pornography’ utakaopiga marufuku uvaaji miniskirts na nguo zingine zinazotamanisha kimapenzi. Muswada huo unaopingwa vikali kama tishio kwa haki za wanawake, unaweza kufanya filamu nyingi na tamthilia kupigwa marufuku.

8414788864_1df97240fd_o

Wengine wanasema muswada huo unaweza kuzuia video nyingi za wasanii kama Beyonce ama Rihanna kuchezwa kwenye runinga za nchini humo.

Rihanna

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor muswada huo unapiga marufuku kitu chochote kinachoonesha sehemu za faragha kama matiti, mapaja na makalio ama tabia yoyote inayoweza kuamsha hisia za mapenzi au tabia yoyote inayoenda kinyume na maadili.

Muswada huo umekuja kufuatia kuongezeka kwa masuala ya pornography nchini Uganda ni marudio ya kile kilichofanyika wakati wa uongozi wa Idi Amin aliyepiga marufuku uvaaji wa sketi fupi miaka 1970s.

Leo pia wabunge wa nchi hiyo wamepitisha muswada wa kuzuia ushoga nchini humo. Muswada huo unapendekeza kifungo cha maisha kwa mashoga au kifo kwa wale wanaorudia makosa hayo. Kama muswada huo ukipita, mtu yeyote atakayeshindwa kumripoti mtu anayejulikana kuwa shoga naye anaweza kushtakiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents