Michezo

Mashabiki wa Yanga kupata Simu kwa Mkopo

Klabu ya Yanga SC imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Silver General Investment ambapo mashabiki wa timu hiyo watakopeshwa simu na kulipa kwa awamu.

“Mwanachama na shabiki wa Young Africans ambaye anahitaji kukopeshwa simu anapaswa kutoa kiasi cha Tsh 75,000 na kiasi kinachobaki analipa kidogo kidogo”, amesema Rais wa timu hiyo, Hersi Said katika hafla ya utiaji saini mkataba huo,.

Iliyofanyika leo. Hersi amesema ndani ya simu itakayokopeshwa kutapatikana App ya Yanga SC ambayo imelipiwa kwa miezi miwili na nusu na ametoa wito kwa wanachama kuikimbilia fursa hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Silver General Investment Jerry Onassa ameipongeza Yanga kwa kuwarahisishia mashabiki na wanachama wake kupata simu hizo…..

“Naipongeza Klabu ya Young Africans SC kwa mapinduzi haya ya kuthamini Wanachama na Mashabiki wake kwa kuwarahisishia mfumo mzuri wa wao kupata simu hizi za smartphone. Haya ni mapinduzi makubwa ya kidigitali kwa Klabu.

Asanteni kwa kuungana nasi na tutawahakikishia kuwapa ushirikiano mzuri”, amesema Jerry.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents