Habari

Master J: Studio zimekua nyingi kama Salon, Muziki haulipi


Producer mkongwe na mmiliki wa studio ya Mj Records Joakim Kimaryo aka Master J, amesema studio za muziki zimekuwa nyingi mno kiasi cha kufanya biashara hiyo kuwa ngumu.
Alisema ongezeko la studio za kurekodi muziki nchini ambazo hazina bei moja inayofanana limefanya biashara ya muziki kuzorota kila kukicha.
Akiongea na kipindi cha Bongo Fleva cha Clouds FM jana, Master J ambaye pia ni jaji wa Bongo Star Search aliongeza kuwa tatizo kubwa linatokana na kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya wamiliki/maproducer wa studio hizo ili kupanga bei moja ya kurekodia.
“Kuna studio zinarekodi wimbo mpaka kwa elfu 40,” alisema. Alieleza kuwa studio zingekuwa na ushirikiano kama wa makampuni ya simu Ambayo hukubaliana kiwango cha kuanzia na hata kama mmoja akiongeza bei kutokana na ubora wa huduma yake kiwango cha kuanzia (minimum price) kinabakia pale pale.
Alitolea mfano kuwa kama Marco Chali ambaye anarekodi wimbo mmoja kwa shilingi laki tano akizidiwa uwezo na Lamar, hakuna ubaya Lamar kuchaji shilingi laki saba kwakuwa uwezo wake ni mkubwa na hitaji la production zake ni kubwa pia.
Katika hatua nyingine Master J ambaye studio yake ni miongoni wa studio zinazofanya matangazo kibao ya biashara nchini, alisema zamani wakati studio zinaanza walikuwa wanarekodi bure.
Alisema anakumbuka hela kubwa aliyoipata miaka hiyo ni kutoka kwa Joseph Mbilinyi aliyekuwa anajulikana zaidi kama Mr Two aliyerekodi albam yake na kumlipa shilingi ‘elfu tano’ kwa wimbo mmoja.
Aliongeza kuwa muziki wa Bongo Fleva kipindi hicho ulikuwa ukipigwa na radio moja tu ambapo hata hivyo nyimbo hizo zilipigwa ndani ya dakika tano za mwisho wa kipindi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents